.
Saturday, August 10, 2013 | 3:54 PM
Yobnesh Yusuph(Batuli) ambaye ni actress maarufu Swahiliwood amemuomba
Rais Jakaya Kikwete alivunje Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) na
kuliunda upya. Leo kupitia akaunti yake ya twitter muigizaji huyo
aliyejaaliwa mvuto na kupendwa na mashabiki wengi wa filamu ali-tweet
moja kwa moja akimtaja JK kwa kuandika "ujumbe wa sikukuu ya Eid kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana, vunja baraza la BASATA uliunde upya".
Ingawa Batuli hakutaja moja kwa moja kwanini baraza hilo linalosimamia
sanaa ikiwemo tasnia ya filamu nchini livunjwe lakini kwa muda mrefu
wasanii wakiwemo wa filamu na muziki wamekuwa wakililalamikia baraza
hilo kuwa linafanya mambo kienyeji na baadhi ya wasanii kudai kukumbana
na urasimu wanapotaka kufanya kazi zao za sanaa.
Wengine wanadai hata hatua iliyopigwa sasa katika sanaa nchini ni juhudi
za wasanii wenyewe pasipo sapoti ya kutosha kutoka BASATA. Baadhi ya
wasanii wa filamu wamekuwa pia wakitaka TAFF ndiyo ipewe mamlaka kamili
ya kusimamia shughuli zote za tasnia ya filamu nchini kutokana na
BASATA kuwepo muda mrefu lakini Sanaa ya Tanzania bado haijapewa hadhi ya
sekta rasmi na kuwa na sera ya kueleweka katika kumkomboa msanii na
kuzidi kupiga hatua.
Hivi karibuni pia mwanamuziki Diamond Platinumz alikaririwa akisema
BASATA ndiyo wa kulaumiwa kwa kutokuwa na tuzo nyingine za muziki mpaka
sasa kwa kuwa chombo hicho kimekuwa kikiweka kauzibe kwa watu wanaotaka
kuazisha tuzo mbalimbali za sanaa ikiwemo hata katika tasnia ya filamu.
No comments:
Post a Comment