EFA ALIYEMLIMA NYEKUNDU RONALDO AFUNGIWA MWEZI MMOJA NA KUPIGWA STOP KABISA KUCHEZESHA MECHI ZA REAL MADRID
REFA
aliyemuonyesha kadi nyekundu Cristiano Ronaldo wakati Real Madrid
ikitoa sare na Athletic Bilbao mwishoni mwa wiki iliyopita amefungiwa
kwa sababu za kuvurunda katika maamuzi yake.
Kamati
ya Ufundi ya Marefa Hispania (CTA) limemfungia kwa mwezi mmoja Miguel
Angel Ayza Gamez na hataruhusiwa kabisa kuchezesha mechi za Real msimu
huu.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Hispania, kuna hatari zaidi akaondolewa kabisa
katika orodha ya marefa wa La Liga kutokana na madudu aliyoyafanya
katika mechi hiyo.
Mdogo mdogo: Ronaldo akiondoka taratibu uwanjani baada ya kulimwa nyekundu
Ronaldo
alitolewa nje kwa mara ya saba katika historia yake ya soka dakika ya
75 siku hiyo timu hizo zikifungana 1-1 Uwanja wa San Mames baada ya
kumuinulia mkono Nahodha wa Bilbao, Carlos Gurpegi, ambaye alijiangusha.
Pia alimvaa kiungo wa Bilbao, Ander Iturraspe wakati akiwa na hasira za tukio hilo.
Inafahamika
taarifa ya awali ya Ayza Gamez ilisema alimtoa nje Ronaldo kwa tulio
alilolifanya kwa Gurpegi, lakini baadaye akabadilisha na kusema alimtoa
nje kwa kosa la kumsukuma Iturraspe - maneno ambayo yalisemwa na
mchezaji huyowa Bilbao.
No comments:
Post a Comment