HIKI ni kioja! Ndugu wa marehemu Elitha
Kaizilege ambaye alipatwa na mauti katika Hospitali ya Kairuki iliyopo
Mikocheni jijini Dar wiki iliyopita, walifanya tukio la aina yake baada
kutokukubali kama ndugu yao amefariki.
Kana kwamba haitoshi, baada ya muda huo kupita, ndugu hao, wanaosadikika kuwa ni waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima, waliupeleka kanisani hapo ambapo uliombewa zaidi ya saa mbili mwili huo ili uamke, ikashindikana.
Wakati akiumwa, inadaiwa kuwa tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ni sikio lakini katika vipimo kadhaa alivyopimwa, havikuonyesha ugonjwa.
Kwa mara ya mwisho kuna madai kuwa alikuwa na kansa ya kichwa, kitu ambacho pia kiliwashangaza ndugu ambao walishangaa ni wapi alipoutoa ugonjwa huo mara moja.
Inasemekana kuwa mara tu baada ya madaktari wa Hospitali ya Kairuki kuwataarifu kuhusu kifo cha mgonjwa wao, walizuia mwili huo kupelekwa chumba cha maiti wakiamini hajafariki, na kwamba wanataka wafanye maombi ili kumfufua.
Baada ya maombi ya hospitalini na kanisani kushindikana, mchungaji aliyeongoza ibada hiyo, ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja, aliwaambia ndugu hao kuwa marehemu hataweza kuamka na kuwataka waupeleke mwili huo chumba cha kuhifadhia maiti.
Waandishi wetu walimtafuta kiongozi mkuu wa kanisa hilo mchungaji Josephat Gwajima ili aweze kuzungumzia suala hilo, lakini waliambiwa kuwa yuko Japan kwa kazi ya kuhubiri neno.
Hata hivyo, mmoja wa viongozi waandamizi wa kanisa hilo, aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema maombi ya aina hiyo hufanyika kanisani hapo na mara kadhaa, watu waliodhaniwa wamefariki waliweza kuinuka
Ndugu wa marehemu Elitha Kaizilege wakipeleka mwili wa ndugu yao kanisani kwa ajili ya maombi.
Ndugu hao wa marehemu walizuia mwili huo
kupelekwa mochwari na badala yake wakauombea kwa saa sita hospitalini
hapo wakiamini ataamka, kwani ugonjwa wake ni wa kulogwa.Kana kwamba haitoshi, baada ya muda huo kupita, ndugu hao, wanaosadikika kuwa ni waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima, waliupeleka kanisani hapo ambapo uliombewa zaidi ya saa mbili mwili huo ili uamke, ikashindikana.
Mchungaji Gwajima akiwa kazini.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, marehemu
ambaye alirejea nchini hivi karibuni kutoka Marekani alikoenda
kuhudhuria mahafali ya mwanaye anayesoma nchini humo, alianza kuumwa
kimasihara, hasa kwa vile ugonjwa wake ulikuwa haueleweki licha ya
kupelekwa katika hospitali mbalimbali jijini.Wakati akiumwa, inadaiwa kuwa tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ni sikio lakini katika vipimo kadhaa alivyopimwa, havikuonyesha ugonjwa.
Kwa mara ya mwisho kuna madai kuwa alikuwa na kansa ya kichwa, kitu ambacho pia kiliwashangaza ndugu ambao walishangaa ni wapi alipoutoa ugonjwa huo mara moja.
Mchungaji Gwajima katika harakati ya kumtoa mapepo mgonjwa.
Inadaiwa pia kuwa wakati akiumwa, mama
huyo aliwahi kupigiwa simu na mtu anayehisiwa ni mganga wa kienyeji
kutoka Kigoma, ambaye haikufahamika walichoongea.Inasemekana kuwa mara tu baada ya madaktari wa Hospitali ya Kairuki kuwataarifu kuhusu kifo cha mgonjwa wao, walizuia mwili huo kupelekwa chumba cha maiti wakiamini hajafariki, na kwamba wanataka wafanye maombi ili kumfufua.
Baada ya maombi ya hospitalini na kanisani kushindikana, mchungaji aliyeongoza ibada hiyo, ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja, aliwaambia ndugu hao kuwa marehemu hataweza kuamka na kuwataka waupeleke mwili huo chumba cha kuhifadhia maiti.
Waandishi wetu walimtafuta kiongozi mkuu wa kanisa hilo mchungaji Josephat Gwajima ili aweze kuzungumzia suala hilo, lakini waliambiwa kuwa yuko Japan kwa kazi ya kuhubiri neno.
Hata hivyo, mmoja wa viongozi waandamizi wa kanisa hilo, aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema maombi ya aina hiyo hufanyika kanisani hapo na mara kadhaa, watu waliodhaniwa wamefariki waliweza kuinuka
No comments:
Post a Comment