Sunday, August 11, 2013 | 12:52 AM
OFISA wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
(TAA), aliyekuwa zamu siku dawa za kulevya zilipopitishwa katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na kukamatwa
Afrika Kusini amesimamishwa kazi.
Dawa hizo zilipitishwa na wanawake
wawili zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6.8 wakitoka nchini
ambapo ofisa aliyekuwa sehemu ya kukagua mizigo alihusishwa na
kusimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Jeshi la
Polisi, Said Mwema alipozungumza na waandishi wa habari na kusema baada
ya uchunguzi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
Hata hivyo hakutaja ofisa huyo
aliyesimamishwa kazi. Wanawake waliokamatwa na dawa hizo ni Agnes Gerald
(25) na Melisa Edward (24) ambao walifunguliwa mashitaka Afrika Kusini.
Walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya
Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalikaguliwa na
kukutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kwa
jina la ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya randi milioni 42
sawa na Sh bilioni 6.8.
Kusimamishwa kazi kwa ofisa huyo ni
mikakati ya Polisi kuhakikisha kurejeshwa kwa sifa ya kuaminika kwani
sasa inatajwa kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
kuwa ni moja ya njia kuu za kusafirisha dawa za kulevya.
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Elieza
Feleshi, alisema katika kuhakikisha haki inatendeka, hawezi kuwakingia
kifua watendaji wabovu na kuahidi kuwashughulikia kutokana na mashitaka
waliyonayo.
Alisema baada ya kuwapo tuhuma kwamba amekuwa akiwakingia kifua watendaji wabovu jambo ambalo alisema si kweli.
Aidha, alisisitiza kuwa si kweli kwamba
kuna taarifa za watu kubambikiwa kesi kwani haki inatendeka kwa
watuhumiwa wote, jambo lililosaidia kupunguza mlundikano wa wafungwa
kutoka 45,000 hadi 33,000 wiki hii
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/08/sakata-la-dawa-za-kulevya-lazidi.html#ixzz2bbiQhR7B
No comments:
Post a Comment